KAGERA CO-OPERATIVE UNION (1990) LTD

Chama kikuu cha ushirika cha Kagera Cooperative Union (1990) LTD ni chama kilichoandikishwa chini ya Sheria ya Vyama vya Ushirika Na. 6 ya mwaka 2013 pamoja na Kanuni zake za mwaka 2015. Kwa mwaka huu 2025/2026, Chama kimetenga fedha kwa ajili ya kumpata mtaalamu mbobevu wa kuandaa michoro, gharama za kazi pamoja na kuwa mtaalamu mwelekezi wa kazi za kutengeneza mazingira ya kiwanja cha ukumbi wa KCU Conference Center (KCC). Kazi hii itafanyika bada ya kukamilisha ujenzi wa uzio na mtaro wa mto unaokatiza kiwanja cha ukumbi wa KCC.

 

SIFA ZA MWOMBAJI
1. Mtaalamu katika muundo wa mazingira au uwanda unaohusiana .
2. Awe na uwezo wa kupanga, kubuni na kushauri kuhusu ujenzi wa mazingira ya umma.
3. Awe na uzoefu wa kufanya, kushauri na kusimamia kazi zinazo husiana na mazingira.

 

Waombaji wenye sifa wanakaribishwa kufika ofisini na kuonana na Afisa Manunuzi kwa ajili ya kupelekwa saiti na kuoneshwa maeneno husika.
Siku ya kutembelea eneo la mradi ni tarehe 26/05/2025 siku ya Jumatatu kuanzia saa 4.00 asubuhi. Safari itaanzia ofisi kuu KCU (1990) LTD.
Ufafanunuzi wa nini kinahitajika kutoka kwa mtaalamu mlengwa (TOR) unapatikana ofisini kwa Afisa Manunuzi KCU (1990) LTD siku za kazi kuanzia tarehe 19/05/2025 hadi tarehe 02/06/2025 saa 3:00 asubihi hadi saa 10:00 jioni baada kulipa ada ya maombi ya zabuni Tsh 50,000/= na kupatiwa stakabadhi ya malipo. Fedha zilipwe katika AC No 01J1055955002 iliyoko CRDB Bank kwa jina la KCU General A/C

 

NAMNA YA KUWASILISHA MAOMBI
Barua za maombi zifungwe katika bahasha moja kwa lakiri na kuandikwa juu yake:- “MAOMBI YA USHAURI KWA AJILI YA KUMPATA MTAALAMU MBUNIFU WA MAZINGIRA KWA AJILI YA KUANDAA MICHORO, GHARAMA ZA KAZI(BOQ) PAMOJA NA KUWA MTAALAMU MWELEKEZI WA MRADI WA KUTENGENEZA MAZINGIRA YA KIWANJA CHA UKUMBI WA KCU CONFERENCE CENTER(KCC)

Maombi yatumwe kwa anuani tajwa hapa chini:-

MENEJA MKUU,
KCU (1990) LTD,
P.O BOX 5,
BUKOBA.

 

Bahasha hiyo iletwe katika Ofisi ya Manunuzi KCU kabla au mnamo tarehe 03/06/2025 saa
4.00 asubuhi siku ya Jumanne na ufunguzi wa maombi yote utafanyika muda huo. Waombaji au
wawakilishi wa waombaji wanaalikwa kuhudhuria sherehe ya ufunguzi mara tu baada ya saa ya
mwisho ya kupokea zabuni.
Maombi yatakayo chelewa, maombi yasiyokamilika, maombi yaliyowasilishwa kwa njia ya
kieletroniki na maombi yasiyokuwepo siku ya ufunguzi hayatahusishwa na uchambuzi wa
kumpata mzabuni.

Imetolewa na;

 


MENEJA MKUU
KCU (1990) LTD

Kwa Taarifa zaidi, Bofya Kittufe  cha Pakua

19.05.2025
landscape designer