Kagera Cooperative Union (1990) Limited

TENDER

KAGERA CO-OPERATIVE UNION (1990) LTD

Kagera cooperative union (1990) LTD (KCU (1990) LTD) inawatangazia wananchi wote, watu binafsi na makampuni ya ndani ya nchi kuomba zabuni ya kupangishwa Bahaya Lodge iliyopo katika jengo la ghorofa ya 3 na ya 4 katika jengo liitwalo Bahaya kiwanja No. 24 BLOCK J – Bukoba Manispaa. Jengo linatumika kwa matumizi ya biashara ya lodge kwa maana ya kupangisha vyumba vya kulala wageni.

MASHARTI YA ZABUNI

  1. Mwombaji ataje kodi ya kupangishwa kwa mwezi.
  2. Mwombaji anatakiwa kulipa ada ya zabuni kiasi cha Tsh 100,000 ambayo haitarudishwa. Fedha zilipwe katika benki ya CRDB akaunti no 01J1055955002 -Kagera cooperative Union, General Account
  3. Mwombaji atapewa nyaraka za maombi zinazopatikana katika ofisi ya manunuzi baada ya kulipa ada ya zabuni siku za kazi kuanzia Jumatatu hadi Ijumaa saa 2.30 asubuhi hadi 10.00 alasiri.
  4. Mwombaji anatakiwa kuomba kupangishwa lodge hii baada ya kusoma na kuelewa hadidu za rejea ambazo zinapatikana ofisi ya manunuzi baada ya kulipia ada ya zabuni.
  5. Mwombaji atakayeshinda zabuni hii ataingia mkataba na KCU (1990) LTD mara baada ya kulipia kodi ya pango ya miezi kumi na miwili (12) na wekesho (deposit) ya kodi ya pango ya miezi sita (6).
  6. Mwombaji atatakiwa kutumia jengo hili kwa matumizi ya lodge tu na si vinginevyo.
  7. Mwombaji atawajibika kulinda mali za KCU (1990) LTD atakazokabidhiwa ikiwa ni pamoja na kutunza jengo na mazingira yake katika hali ya unadhifu.
  8. Mwombaji anapaswa kuwa na viambatisho vifuatavyo: –
  • Leseni hai ya biashara
  • Kitambulisho cha mlipa kodi (TIN Namba)
  • Kama ni mtu binafsi wasifu wake utakaoambata na picha binafsi ya passport size.
  • Kama ni kampuni ya ndani, mwombaji aambatishe hati ya kujasiliwa Brella pamoja na MEMARTS za kampuni.
  1. Tathmini itafanyika kwa kuzingatia kigezo namba 1 hadi 8 hapo juu.
  2. Maombi yaletwe kwa mkono yakiwa yamefungwa vizuri kwenye bahasha na kufikishwa ofisi ya manunuzi KCU (1990) LTD. Mwisho wa kutuma maombi ni siku ya Alhamisi Tarehe 15.01.2026 saa nne kamili asubuhi.  Juu ya bahasha paandikwe “MAOMBI YA KUPANGISHWA BAHAYA LODGE”.Ufunguzi wa barua zote utafanyika muda na siku hiyo na waombaji wanaweza kuhudhuria wakati wa ufunguzi.
  3. Siku ya kutembelea hoteli inayopangishwa ni  tarehe 08.01.2026 saa 4.00 asubuhi. Waombaji wawe wamefika ofisi kuu KCU (1990) LTD muda huo tayari kuondoka kwa pamoja kwenda kwenye hoteli inayopangishwa.

 

  1. Barua zote za maombi ziandikwe kwa anuani ifuatayo: –

MENEJA MKUU,

KCU 1990 LTD,

BOX 5,

BUKOBA.

 

Imetolewa na:-

MENEJA MKUU

KCU (1990) LTD

Ili kuona Tangazo kamili, tafadhali bofya kiunganishi hapo chini ili kupakua Tangazo:

31.12.2025
Tangazo la kupangisha Bahaya Lodge