Kagera Cooperative Union (1990) Limited

MIRADI

Kagera cooperative union (1990) LTD (KCU (1990) LTD) inawatangazia wananchi wote, watu binafsi na makampuni ya ndani ya nchi kuomba zabuni ya kupangishwa Bahaya Lodge iliyopo katika jengo la ghorofa ya 3 na ya 4 katika jengo liitwalo Bahaya kiwanja No. 24 BLOCK J – Bukoba Manispaa. Jengo linatumika kwa matumizi ya biashara ya lodge kwa maana ya kupangisha vyumba vya kulala wageni.

  1. Mwombaji ataje kodi ya kupangishwa kwa mwezi (eleza kama ni pamoja na VAT au bila VAT).
  2. Mwombaji anatakiwa kulipa ada ya zabuni kiasi cha Tsh 50,000 ambayo haitarudishwa. Fedha zilipwe katika benki ya CRDB akaunti no 01J1055955002 -Kagera cooperative Union, General Account
  3. Nyaraka za maombi zinapatikana katika ofisi ya manunuzi KCU 1990 LTD baada ya kulipa ada ya zabuni siku za kazi kuanzia Jumatatu hadi Ijumaa saa 2.30 asubuhi hadi 10.00 alasiri kuanzia tarehe ya tangazo hili. Mwombaji anaweza kutumiwa nyaraka ya zabuni kwa njia ya kidigitali
  4. Mwombaji anatakiwa kuomba kupangishwa lodge hii baada ya kusoma na kuelewa hadidu za rejea ambazo zinapatikana ofisi ya manunuzi na kwa njia ya digitali baada ya kulipia ada ya zabuni.
  5. Mwombaji atatakiwa kutumia jengo hili kwa matumizi ya lodge tu na si vinginevyo.
  6. Mwombaji atawajibika kulinda mali za KCU (1990) LTD atakazokabidhiwa ikiwa ni pamoja na kutunza jengo na mazingira yake katika hali ya unadhifu.
  7. Mwombaji anapaswa kuambatisha viambatisho vifuatavyo: –
  • Nakala ya leseni hai ya biashara
  • Nakala ya kitambulisho cha mlipa kodi (TIN Namba)
  • Kama ni mtu binafsi wasifu wake utakaoambata na picha binafsi ya passport size.
  • Kama ni kampuni mwombaji aambatishe hati ya kujasiliwa BRELLA.
  1. Tathmini itafanyika kwa kuzingatia vigezo namba 1 hadi 8 hapo juu.
  2. Maombi yaletwe kwa mkono yakiwa yamefungwa vizuri kwa lakiri na bahasha kufikishwa ofisi ya manunuzi KCU (1990) LTD. Mwisho wa kuleta maombi ni siku ya Jumatano Tarehe 05.08.2026 saa nne kamili asubuhi  Juu ya bahasha paandikwe “MAOMBI YA KUPANGISHWA BAHAYA LODGE”. Ufunguzi wa barua zote utafanyika muda na siku hiyo na waombaji wanaweza kuhudhuria wakati wa ufunguzi.
  3. Maombi yatakayochelewa au kuletwa baada ya saa ya ufunguzi,maombi yatakayotumwa kwa njia ya kidigitali hayatakubaliwa.
  4. Siku ya kutembelea hoteli inayopangishwa ni  tarehe 29.07.2026 saa 4.00 asubuhi siku ya Jumatano. Waombaji wawe wamefika ofisi kuu KCU (1990) LTD muda huo tayari kuondoka kwa pamoja kwenda kwenye hoteli inayopangishwa. Mwombaji anaweza kutembelea link ifuatayo kwa ajili ya kuona mandhari ya Lodge: https://kcu.or.tz/bahaya-lodge/
  1. Barua zote za maombi ziandikwe kwa anuani ifuatayo: –

MENEJA MKUU,

KCU 1990 LTD,

BOX 5,

BUKOBA.

Imetolewa na:- 

General Manager

KCU (1990) LTD

Kuona Tangazo, Tafadhali bofya kiunganishi hapo chini:-

22.07.2026
bahaya lodge