Kagera Cooperative Union (1990) Limited
Jobs
Jobs
KAGERA CO-OPERATIVE UNION (1990) LTD
KCU (1990) LTD, ni chama kikuu cha ushirika mkoa cha Kagera kinachohudumia wilaya tatu ambazo ni Bukoba, Muleba na Misenyi. Kinatangaza ajira kwa nafasi zifuatazo:
VIGEZO NA UZOEFU.
- Awe na Shahada ya kwanza katika masomo ya uhasibu, fedha na utawala wa biashara kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali.
- Lazima awe na taaluma ya ‘CPA’ katika daraja la ‘Associate/Fellow’
- Awe na walau uzoefu wa miaka mitatu katika kazi ya uhasibu.
- Awe na uwezo wa kushirikiana na wenzake katika kutimiza malengo ya taasisi.
- Awe na uwezo wa kutumia kompyuta pamoja na Mifumo ya TEHAMA.
- Awe na umri wa kuanzia miaka 25 na kuendelea.
- Awe ni raia wa Tanzania.
- Awe hajawahi kuhukumiwa kwa kosa la jinai.
MAJUKUMU YAKE YATAKUWA KAMA IFUATAVYO.
- Mshauri Mkuu wa Meneja Mkuu, Menejimenti na Bodi ya Chama kuhusiana na masuala yote ya fedha;
- Kusimamia idara ya Uhasibu na kufuatilia taarifa za fedha kila siku;
- Kuhakikisha kwamba kazi za kifedha za KCU zinatekelezwa kwa usahihi na kwa mujibu wa sheria na kanuni zilizowekwa;
- Kuratibu zoezi la uandaaji bajeti.
- Kuhakikisha kwamba marejesho yote ya kisheria yameandaliwa na fedha zinazotumwa zinatolewa kwa wakati.
- Kufanya utatuzi wa miamala kwa mujibu wa idhini na kwa kuzingatia busara na udhibiti uliopo wa ndani ya Chama.
- Kutayarisha taarifa za kisheria na udhibiti kulingana na viwango vinavyokubalika vya uhasibu;
- Kutoa mwongozo kwa Menejimenti kuhusu masuala yanayohusu uhasibu pamoja na utoaji wa taarifa za fedha na udhibiti;
- Kutekeleza majukumu mengine kama ilivyoelekezwa na msimamizi wake yanayoendana na kazi yake.
VIGEZO NA UZOEFU.
- Muombaji awe na Stashahada ya Utunzaji kumbukumbu kutoka chuo kinacho tambuliwa na Serikali.
- Awe na uzoefu wa kazi usiopungua miaka miwili.
- Awe ni raia wa Tanzania.
- Awe na Umri wa kuanzia miaka 25 na kuendelea.
- Awe hajawahi kuhukumiwa kwa kosa la jinai.
- Awe na uwezo wa kutumia Compyuta.
MAJUKUMU YAKE YATAKUWA KAMA IFUATAVYO:
- Kutafuta kumbukumbu/Nyaraka/Majalada yanayohitajiwa na Wasomaji.
- Kudhibiti upokeaji, Uandikishaji wa Kumbukumbu/ Nyaraka.
- Kuchambua, Kuboresha, na Kupanga kumbukumbu/Nyaraka/Majarada katika Makundi kulingana na somo husika kwa ajili ya matumizi ya Ofisi.
- Kuweka, kupanga kumbukumbu/Nyaraka, katika reki katika Masijala/ vyumba vya kuhifadhia kumbukumbu.
- Kuweka Kumbukumbu (Barua, Nyaraka muhimu n.k) katika majalada.
- Kupokea Nyaraka za kiofisi.
- Kufanya Shughuli nyinginezo atakazoelekezwa na Uongozi.
VIGEZO NA UZOEFU.
- Awe na Stashahada ya Kilimo/Ubora/ toka chuo kinachotambuliwa na Serikali, Mwenye Cheti cha Uonjaji wa Kahawa atakuwa ana sifa ya ziada.
- Awe na uzoefu wa kazi usiopungua miaka miwili.
- Awe ni raia wa Tanzania.
- Awe na Umri wa kuanzia miaka 25 na kuendelea.
- Awe hajawahi kuhukumiwa kwa kosa la jinai.
- Awe na uwezo wa kutumia Compyuta.
MAJUKUMU YAKE YATAKUWA KAMA IFUATAVYO:
- Kuhakiki ubora wa kahawa.
- Kuhakiki muonjo mzuri wa kahawa.
- Kuandaa sampuli za kahawa na kuziwasilisha mnadani.
- Kukaanga na kusaga Kahawa ya uonjaji kabla ya mnada.
- Kutunza nyaraka na taarifa za sampuli na uonjaji.
- Kuandaa na kutuma sampuli kwa wateja wa ndani na nje ya nchi.
- Kufanya kazi nyinginezo kama zitakavyoelekezwa na kiongozi wake.
MSHAHARA: Ni kulingana na viwango vya Mshahara vya KCU (1990) LTD.
VIAMBATISHO.
Kwa kila muombaji anatakiwa kutuma;
- Barua ya maombi ya kazi iliyosainiwa ikiambatana na Nakala ya cheti cha kuzaliwa na vyeti vya elimu ya Sekondari, pamoja na vyeti vya taaluma vilivyothibitishwa na Mwanasheria.
- Wasifu binafsi (CV).
- Picha ndogo moja pamoja na
- Majina na anwani za wadhamini wake watatu (3).
Barua zote za maombi ya kazi ziandikwe kwa;
Meneja Mkuu,
KCU (1990) LTD,
SLP 5,
BUKOBA.
Mwisho wa kupokea barua za maombi haya ya kazi ni tarehe 08/Februari/2025. Ifikapo saa 4:00 kamili asubuhi.
Kwa taarifa zaidi, Bofya kitufe cha kupakua Tangazo zima.