Kagera Cooperative Union (1990) Limited
MIRADI
Kagera cooperative union (1990) LTD (KCU (1990) LTD) inawatangazia wananchi wote, watu binafsi na makampuni ya ndani ya nchi kuomba zabuni ya kupangishwa Bahaya Lodge iliyopo katika jengo la ghorofa ya 3 na ya 4 katika jengo liitwalo Bahaya kiwanja No. 24 BLOCK J – Bukoba Manispaa. Jengo linatumika kwa matumizi ya biashara ya lodge kwa maana ya kupangisha vyumba vya kulala wageni.
- Mwombaji ataje kodi ya kupangishwa kwa mwezi.
- Mwombaji anatakiwa kulipa ada ya zabuni kiasi cha Tsh 50,000 ambayo haitarudishwa. Fedha zilipwe katika benki ya CRDB akaunti no 01J1055955002 -Kagera cooperative Union, General Account
- Mwombaji atapewa nyaraka za maombi zinazopatikana katika ofisi ya manunuzi baada ya kulipa ada ya zabuni siku za kazi kuanzia Jumatatu hadi Ijumaa saa 2.30 asubuhi hadi 10.00 alasiri.
- Mwombaji anatakiwa kuomba kupangishwa lodge hii baada ya kusoma na kuelewa hadidu za rejea ambazo zinapatikana ofisi ya manunuzi baada ya kulipia ada ya zabuni.
- Mwombaji atatakiwa kutumia jengo hili kwa matumizi ya lodge tu na si vinginevyo.
- Mwombaji atawajibika kulinda mali za KCU (1990) LTD atakazokabidhiwa ikiwa ni pamoja na kutunza jengo na mazingira yake katika hali ya unadhifu.
- Mwombaji anapaswa kuwa na viambatisho vifuatavyo: –
- Leseni hai ya biashara
- Kitambulisho cha mlipa kodi (TIN Namba)
- Kama ni mtu binafsi wasifu wake utakaoambata na picha binafsi ya passport size.
- Kama ni kmapuni mwombaji aambatishe hati ya kujasiliwa BRELLA.
- Tathmini itafanyika kwa kuzingatia kigezo namba 1 hadi 8 hapo juu.
- Maombi yaletwe kwa mkono yakiwa yamefungwa vizuri kwenye bahasha na kufikishwa ofisi ya manunuzi KCU (1990) LTD. Mwisho wa kuleta maombi ni siku ya Jumanne Tarehe 24.02.2026 saa nne kamili asubuhi. Juu ya bahasha paandikwe “MAOMBI YA KUPANGISHWA BAHAYA LODGE”.Ufunguzi wa barua zote utafanyika muda na siku hiyo na waombaji wanaweza kuhudhuria wakati wa ufunguzi.
- Siku ya kutembelea Lodge inayopangishwa ni tarehe 17.02.2026 saa 4.00 asubuhi siku ya Jumanne. Waombaji wawe wamefika ofisi kuu KCU (1990) LTD muda huo tayari kuondoka kwa pamoja kwenda kwenye Lodge inayopangishwa.
- Barua zote za maombi ziandikwe kwa anuani ifuatayo: –
MENEJA MKUU,
KCU 1990 LTD,
BOX 5,
BUKOBA.
Imetolewa na:-
General Manager
KCU (1990) LTD
Kuona Tangazo, Tafadhali bofya kiunganishi hapo chini:-
10.2.2026
bahaya lodge
