Kagera Cooperative Union (1990) Limited

Mfumo wa MUVU

Matumizi ya Mfumo wa MUVU Kukusanya Mazao ya Wakulima katika vyama vya Ushirika

Matumizi ya Mfumo wa Usimamizi wa Vyama vya Ushirika -MUVU umeleta mabadiriko makubwa sana katika Ushirika kwa kuwasaidia wakulima kurahisisha Ukusanyaji wa Mazao (Kahawa) kwa kutumia mizani ya Kidigitali. 

Mfumo wa MUVU pamoja na matumizi ya Mizani  ya Kidigitali imeleta faida zifuatazo kwa Wakulima wa Kahawa na vyama vya Ushirika:-

  1. Uwazi – Mfumo huu umeleata uwazi mkubwa kwa Wakulima kwani Mizani ya Kidigitali inapima na kuonesha kwa tarakimu (digits) tofauti na mizani iliyokuwa ikitumika zamani (Mizani ya Rula). Pamoja na Uwazi wa Usomaji wa Uzito kwenye mzani, Mfumo huu pia unatoa Stakabadhi (Receipt) inayoonesha mchanganuo wa Makusanyo yaliyopimwa kupitia Mizani hiyo pamoja na kutuma Ujumbe Mfupi (SMS) katika simu ya Mkulima. Stakabadhi pamoja na SMS zinazotolewa kwa Wakulima, huwasaidia Wakulima kutumika kama rejea wakati wa kupokea malipo baada ya Mauzo ya Kahawa hizo kwenye Mnada wa Wazi kupitia mfumo wa TMX.
  2. Upatikanaji wa Takwimu sahihi ya Makusanyo ya Kahawa,  Wakulima na Mashamba ya Wakulima. Mfmo huu wa MUVU umesaidia Utunzaji wa Taarifa hizo katika mifumo ya kuhifadhia taarifa (Servers). Hii imerahisisha upatikanaji wa taarifa muda wowote zinapohitajika na zinatunzwa kwa muda mrefu kwa ajili ya matumizi ya baadaye. Upatikanaji wa Taarifa hizi utaisaidia Serikali namna bora ya kutawanya Rasilimali (allocation of Resources) kwa Wakulima kama vile Pembejeo, Miundo mbinu, n.k
  3. Kuondoa Makosa ya Kibinadamu (Human Errors Reduction). Upimaji  wa Mazao kwa Kutumia Mfumo wa Mizani ya Kidigitali (MUVU) umesaidia kuondoa makosa ya Kibinadamu kama vile Upimaji wa Kahawa Hewa kwani Uzito unaopimwa na kuonekana katika Mzani pia unarekodiwa kwenye mfumo moja kwa moja pasipo kuingizwa na Mpimaji ( Weights are Captured Automaticaly by the System).  Kwahiyo kitendo cha Mfumo wenyewe kuwasiliana na mzani na kurekodi mapimo pasipo mwanadamu kuingiza taarifa hizo kumesaidia kuondoa tatizo la Upatikanaji wa Taarifa zisizosahihi zilizokuwa zinaingizwa na Watumishi wa Vyama vya Msingi manually.
  4. Kurahisisha kazi na Kuokoa Muda. Mfumo wa Usimamizi wa Vyama vya Ushirika (MUVU) umerahisisha kazi kwa kuokoa muda kwa kazi za kuandaa Hesabu katika vyama vya ushirika kwani baada ya makusanyo kukamilika hesabu hutengenezwa na mfumo jambo linalosaidia kuleta ufanisi mkubwa na kuokoa muda.
Matumizi ya Mfumo wa Muvu kukusanya Mazao ya Ushirika