Kagera Cooperative Union (1990) Limited

Jobs

KAGERA CO-OPERATIVE UNION (1990) LTD

KCU (1990) LTD, ni chama kikuu cha ushirika mkoa cha Kagera kinachohudumia wilaya tatu ambazo ni Bukoba, Muleba na Misenyi. Kinatangaza ajira kwa nafasi zifuatazo:

VIGEZO NA UZOEFU.

  1. Awe na Shahada ya kwanza katika masomo ya uhasibu, fedha na utawala wa biashara kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali.
  2. Lazima awe na taaluma ya ‘CPA’ katika daraja la ‘Associate/Fellow’
  3. Awe na walau uzoefu wa miaka mitatu katika kazi ya uhasibu.
  4. Awe na uwezo wa kushirikiana na wenzake katika kutimiza malengo ya taasisi.
  5. Awe na uwezo wa kutumia kompyuta pamoja na Mifumo ya TEHAMA.
  6. Awe na umri wa kuanzia miaka 25 na kuendelea.
  7. Awe ni raia wa Tanzania.
  8. Awe hajawahi kuhukumiwa kwa kosa la jinai.

 

MAJUKUMU YAKE YATAKUWA KAMA IFUATAVYO.

  1. Mshauri Mkuu wa Meneja Mkuu, Menejimenti na Bodi ya Chama kuhusiana na masuala yote ya fedha;
  2. Kusimamia idara ya Uhasibu na kufuatilia taarifa za fedha kila siku;
  3. Kuhakikisha kwamba kazi za kifedha za KCU zinatekelezwa kwa usahihi na kwa mujibu wa sheria na kanuni zilizowekwa;
  4. Kuratibu zoezi la uandaaji bajeti.
  5. Kuhakikisha kwamba marejesho yote ya kisheria yameandaliwa na fedha zinazotumwa zinatolewa kwa wakati.
  6. Kufanya utatuzi wa miamala kwa mujibu wa idhini na kwa kuzingatia busara na udhibiti uliopo wa ndani ya Chama.
  7. Kutayarisha taarifa za kisheria na udhibiti kulingana na viwango vinavyokubalika vya uhasibu;
  8. Kutoa mwongozo kwa Menejimenti kuhusu masuala yanayohusu uhasibu pamoja na utoaji wa taarifa za fedha na udhibiti;
  9. Kutekeleza majukumu mengine kama ilivyoelekezwa na msimamizi wake yanayoendana na kazi yake.

VIGEZO NA UZOEFU.

  1. Muombaji awe na Stashahada ya Utunzaji kumbukumbu kutoka chuo kinacho tambuliwa na Serikali.
  2. Awe na uzoefu wa kazi usiopungua miaka miwili.
  3. Awe ni raia wa Tanzania.
  4. Awe na Umri wa kuanzia miaka 25 na kuendelea.
  5. Awe hajawahi kuhukumiwa kwa kosa la jinai.
  6. Awe na uwezo wa kutumia Compyuta.

MAJUKUMU YAKE YATAKUWA KAMA IFUATAVYO:

  1. Kutafuta kumbukumbu/Nyaraka/Majalada yanayohitajiwa na Wasomaji.
  2. Kudhibiti upokeaji, Uandikishaji wa Kumbukumbu/ Nyaraka.
  3. Kuchambua, Kuboresha, na Kupanga kumbukumbu/Nyaraka/Majarada katika Makundi kulingana na somo husika kwa ajili ya matumizi ya Ofisi.
  4. Kuweka, kupanga kumbukumbu/Nyaraka, katika reki katika Masijala/ vyumba vya kuhifadhia kumbukumbu.
  5. Kuweka Kumbukumbu (Barua, Nyaraka muhimu n.k) katika majalada.
  6. Kupokea Nyaraka za kiofisi.
  7. Kufanya Shughuli nyinginezo atakazoelekezwa na Uongozi.

VIGEZO NA UZOEFU.

  1. Awe na Stashahada ya Kilimo/Ubora/ toka chuo kinachotambuliwa na Serikali, Mwenye Cheti cha Uonjaji wa Kahawa atakuwa ana sifa ya ziada.
  2. Awe na uzoefu wa kazi usiopungua miaka miwili.
  3. Awe ni raia wa Tanzania.
  4. Awe na Umri wa kuanzia miaka 25 na kuendelea.
  5. Awe hajawahi kuhukumiwa kwa kosa la jinai.
  6. Awe na uwezo wa kutumia Compyuta.

MAJUKUMU YAKE YATAKUWA KAMA IFUATAVYO:

  1. Kuhakiki ubora wa kahawa.
  2. Kuhakiki muonjo mzuri wa kahawa.
  3. Kuandaa sampuli za kahawa na kuziwasilisha mnadani.
  4. Kukaanga na kusaga Kahawa ya uonjaji kabla ya mnada.
  5. Kutunza nyaraka na taarifa za sampuli na uonjaji.
  6. Kuandaa na kutuma sampuli kwa wateja wa ndani na nje ya nchi.
  7. Kufanya kazi nyinginezo kama zitakavyoelekezwa na kiongozi wake.

MSHAHARA: Ni kulingana na viwango vya Mshahara vya KCU (1990) LTD.

VIAMBATISHO.

Kwa kila muombaji anatakiwa kutuma;

  • Barua ya maombi ya kazi iliyosainiwa ikiambatana na Nakala ya cheti cha kuzaliwa na vyeti vya elimu ya Sekondari, pamoja na vyeti vya taaluma vilivyothibitishwa na Mwanasheria.
  • Wasifu binafsi (CV).
  • Picha ndogo moja pamoja na
  • Majina na anwani za wadhamini wake watatu (3).

 

Barua zote za maombi ya kazi ziandikwe kwa;

 

Meneja Mkuu,

KCU (1990) LTD,

SLP 5,

BUKOBA.

 

Mwisho wa kupokea barua za maombi haya ya kazi ni tarehe 08/Februari/2025. Ifikapo saa 4:00 kamili asubuhi.

Kwa taarifa zaidi, Bofya kitufe cha kupakua Tangazo zima.

08.01.2025
Tangazo la Kazi