Kagera Cooperative Union (1990) Limited

TENDER

KAGERA CO-OPERATIVE UNION (1990) LTD

Kagera cooperative union (1990) LTD (KCU (1990) LTD) inawatangazia wananchi wote, watu binafsi na makampuni ya ndani nan je ya nchi kuomba zabuni ya kupangishwa Hotel ya Bukoba Coop iliyopo viwanja No. 189, 190, 192, na 193 Block LDA Custom Road- Bukoba Manispaa. Eneo linatumika kwa matumizi ya Hoteli kwa maana ya vyumba, mgahawa, majiko, sehemu za mikutano na sherehe mbalimbali, Baa na eneo la kuegesha magari.

MASHARTI YA ZABUNI

  1. Mwombaji ataje kodi ya kupangishwa kwa mwezi.
  2. Mwombaji anatakiwa kulipa ada ya zabuni kiasi cha Tsh 200,000 ambayo haitarudishwa. Fedha zilipwe katika benki ya CRDB akaunti no 01J1055955002 -Kagera cooperative Union, General Account
  3. Mwombaji atapewa nyaraka za maombi zinazopatikana katika ofisi ya manunuzi baada ya kulipa ada ya zabuni siku za kazi kuanzia Jumatatu hadi Ijumaa saa 2.30 asubuhi hadi 10.00 alasiri.
  4. Mwombaji anatakiwa kuomba kupangishwa hoteli hii baada ya kusoma na kuelewa hadidu za rejea ambazo zinapatikana ofisi ya manunuzi baada ya kulipia ada ya zabuni.
  5. Mwombaji atakayeshinda zabuni hii ataingia mkataba na KCU (1990) LTD mara baada ya kulipia kodi ya miezi kumi na miwili (12) na wekesho (deposit) ya kodi ya miezi sita (6).
  6. Mwombaji atatakiwa kutumia jengo hili kwa matumizi ya Hotel tu na si vinginevyo.
  7. Mwombaji atawajibika kulinda mali za KCU (1990) LTD atakazokabidhiwa ikiwa ni pamoja na kutunza jengo na mazingira yake katika hali ya unadhifu.
  8. Mwombaji anapaswa kuwa na viambatisho vifuatavyo: –
  • Leseni hai ya biashara
  • Kitambulisho cha mlipa kodi (TIN Namba)
  • Kama ni mtu binafsi wasifu wake
  • Kama ni kampuni ya ndani, mwombaji aambatishe hati ya kujasiliwa Brella pamoja na MEMARTS za kampuni.
  • Kama ni kampuni ya kigeni iwe imesajiliwa kama ‘’foreign company’’ kupitia Brella, iwe na TIN, iwe na akaunti ya benki hapa nchini, na ipate uthibitisho kama mwekezaji kutoka kituo cha uwekezaji (TIC)
  1. Tathmini itafanyika kwa kuzingatia kigezo namba 1 hadi 8 hapo juu.
  2. Maombi yaletwe kwa mkono yakiwa yamefungwa vizuri kwenye bahasha na kufikishwa ofisi ya manunuzi KCU (1990) LTD. Mwisho wa kutuma maombi ni siku ya Alhamisi Tarehe 15.01.2026 saa nne kamili asubuhi.  Juu ya bahasha paandikwe “MAOMBI YA KUPANGISHWA HOTELI YA BUKOBA COOP”.Ufunguzi wa barua zote utafanyika muda na siku hiyo na waombaji wanaweza kuhudhuria wakati wa ufunguzi.
  3. Siku ya kutembelea hoteli inayopangishwa ni  tarehe 08.01.2026 saa 4.00 asubuhi. Waombaji wawe wamefika ofisi kuu KCU (1990) LTD muda huo tayari kuondoka kwa pamoja kwenda kwenye hoteli inayopangishwa.

 

  1. Barua zote za maombi ziandikwe kwa anuani ifuatayo: –

MENEJA MKUU,

KCU 1990 LTD,

BOX 5,

BUKOBA.

 

Imetolewa na:-

MENEJA MKUU

KCU (1990) LTD

Ili kuona Tangazo kamili, tafadhali bofya kiunganishi hapo chini ili kupakua Tangazo:

31.12.2025
Zabuni ya kupangisha Hoteli ya Bukoba coop